ICIMAS ni kifupisho cha Integrated Congregation Information Management System, ikimaanisha mfumo wa kidigitali wa kutunza taarifa na kuendesha shughuli za Umoja wa Mashirika ya Kitawa nchini (TCAS yaani Tanzania Catholic Association of Sisters).
ICIMAS ni mfumo wa ki-mtandao unaoiwezesha TCAS kama mwavuli wa Mashirika ya Kitawa kusimamia, kudhibiti na kuendeleza ustawi wa huduma na shughuli za kitume na kijamii za Mashirika hayo.
Mfumo huu unalenga kuleta mapinduzi katika utendaji wa TCAS na Mashirika yake kwa kurahisisha ubadilishanaji wa taarifa na mawasiliano kati ya TCAS na wanachama wake, utunzaji wa kumbu kumbu, udhibiti na utoaji wa Ripoti na Takwimu katika kuendeleza huduma za kitume na shughuli mbali mbali za maendeleo ya jamii zinazofanywa na Mashirika hayo.
Mfumo huu umezingatia mnyororo wa utendaji (Chain of Service) wa TCAS na Mashirika wanachama kwa kuiwezesha TCAS kutunza taarifa za shughuli zake, kutengeneza takwimu na ripoti mbali mbali lakini pia kupata taarifa za huduma zinazofanywa na mashirika hayo katika maeneo mbali mbali nchini.
Kwa muhtasari ICIMAS inawezesha mambo yafuatayo:-
Kutoa taarifa na takwimu mbali mbali za Watawa katika Mashirika kwa kuzingatia vigezo mbali mbali kama vile: umri, elimu, taaluma n. k.
Kutoa taarifa na takwimu mbali mbali za Miradi ya Maendeleo ya Jamii za Mashirika
Ulipaji wa Mishahara na Udhibiti wa Bajeti za kuendesha taasisi mbali mbali katika Mashirika
Kutunza kumbu kumbu ya shughuli za Uwekezaji na Uzalishaji mali za Mashirika
Kukokotoa na kuonyesha Mapato na Matumizi katika Miradi ya Uwekezaji
Kuzalisha Ripoti za Fedha kwa viwango vya kimataifa (IFRS) mfano: Leja Kuu, Urari, Mizania,nk
Tafadhali ingiza namba yako ya uanachama na nywila yako
Exception caught:An exception occurred processing [/menu/fpwd.jsp] at line [137]
134:
135:
136: <%
137: ResultSet rs3=statement.executeQuery("select * from loan where loan_name='Mkopo wa Dharura'");
138: if(!rs3.next()){
139: %>
140: